Download Music Audio and Video with Ease Using Our Platform

FISA MAENDELEO YA JAMII MSAIDIZI DARAJA II at Halmashauri ya Manispaa ya Musoma February, 2021

Share this

POST AFISA MAENDELEO YA JAMII MSAIDIZI DARAJA II – 1 POST
POST CATEGORY(S) SOCIOLOGY, POLITICAL SCIENCE, COMMUNITY AND SOCIAL DEVELOPMENT
EMPLOYER Halmashauri ya Manispaa ya Musoma
APPLICATION TIMELINE: 2021-02-19 2021-03-04
JOB SUMMARY NA
DUTIES AND RESPONSIBILITIES
i.Kuratibu shughuli zote za maendeleo ya jamii katika Kijiji zikiwemo za Wanawake na Watoto na zikizingatia jinsia;

ii.Kuwezesha jamii kushiriki katika kubuni, kupanga, kutekeleza, kusimamia, kutathmini mipango/miradi ya maendeleo;

iii.Kuhamasisha na kuwawezesha wananchi kupanga na kutekeleza kazi za maendeleo ambazo ni pamoja na usafi wa mazingira, ujenzi wa nyumba bora vijijini, ujenzi wa Shule, Zahanati, Majosho, barabara za vijijini (Feeder Roads), uchimbaji wa visima vifupi na uchimbaji wa marambo;

iv.Kuhamasisha na kuwawezesha wananchi kupanga mbinu za kutatua vikwazo vya maendeleo hasa vya maji na nishati kwa kuwa na miradi ya uvunaji wa maji ya mvua, majiko sanifu na matumizi ya mikokoteni;

v.Kutoa na kuwezesha upatikanaji wa mafunzo kwa viongozi wa Kijiji na vikundi mbalimbali vya maendeleo kijijini kuhusu:-

-Utawala Bora na Uongozi

-Ujasiriamali

-Mbinu shirikishi jamii na kazi za kujitegemea

-Chakula bora na lishe

-Utunzani na malezi bora ya watoto

vi.Kuwa kiungo kati ya wanakijiji (Afisa Mtendaji wa Kata) na watumishi wengine wa Serikali katika kutekeleza shughuli za maendeleo;

vii.Kuwawezesha wananchi kupanga na kutekeleza kazi za kujitegemea;

viii.Kuwawezesha wananchi kubaini na kuratibu rasilimali zilizopo na kuzitumia katika miradi ya kujitegemea;

ix.Kukusanya, kutunza, kutafsiri na kuwasaidia wananchi kutumia takwimu na kumbukumbu mbalimbali za kijiji;

x.Kuwawezesha viongozi wa vijiji kutumia mbinu shirikishi jamii kuandaa ratiba za kazi na mipango ya utekelezaji;

xi.Kuandaa na kutoa taarifa za kazi za maendeleo ya jamii kila mwezi kwa uongozi wa kijiji na kwa Afisa Maendeleo ya Jamii ngazi ya Kata;

xii.Kuhamasisha na kuwezesha jamii kuona umuhimu wa kuthamini mazingira kwa kutumia mazingira kwa njia endelevu na hasa kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji kwa matumizi ya vizazi vya sasa na vya baadae;

xiii.Kusaidia kuunda vikundi vya kijamii na vya kimaendeleo;

xiv.Kuratibu shughuli za Mashirika na Asasi zisizo za Kiserikali na za kijamii;

xv.Kuratibu shughuli za kupambana na UKIMWI.

 

QUALIFICATION AND EXPERIENCE
Wahitimu wa Kidato cha Nne au cha Sita wenye Stashahada ya Maendeleo ya Jamii kutoka Vyuo vya Maendeleo ya Jamii (Buhare au Rungemba) au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.

 

 

 

REMUNERATION TGS C

The deadline for submitting the application is 04 March 2021

CLICK HERE TO APPLY

If you liked this article, then please subscribe to our FREE Job Alerts. You can also find us on Twitter, Instagram and Facebook.
Share this
Only candidates can apply for this job.
Company Information

Search Job here
Jobs in Tanzania: JOB SCAM ALERT!! Never Pay To Get A Job. Legitimate companies don’t ask for money and any employment or job openings with requests for payment or fees should be treated with extreme caution, viewed as potentially fraudulent and reported TO TAKUKURU (PCCB) immediately. Mabumbe.com is not responsible for monies paid to Scammers.

JOBS BY CATEGORIES / FIELD

JOBS VACANCIES BY LOCATION